Kwa mujibu wa kitengo cha tarjama cha Shirika la Habari la Hawza, sambamba na kumbukumbu ya siku ya kuhuzunisha ya kubomolewa kwa makaburi ya kihistoria ya Jannatul-Baqi’, kikao cha kimataifa kilifanyika katika ukumbi wa Shahidi ‘Aref Husseini uliopo katika shule ya Imam Khomeini (r.a) katika mji mtukufu wa Qom, kwa ushiriki wa wasomi na sura mashuhuri kutoka mataifa mbalimbali. Mkutano huu umeandaliwa kwa jitihada za kituo cha kitamaduni cha "Tahrir Post" kwa kushirikiana na taasisi za kiislamu na kielimu kama vile Jumuiya ya Al-Yasin na Kituo cha Afkar Islaami cha India.
Katika mkutano huu, wazungumzaji walilaani vikali hatua dhalimu za kubomoa makaburi ya wana wa Mtume Muhammad (s.a.w), na wakatoa wito wa kufanyika ukarabati wa haraka wa makaburi hayo matukufu. Pia walisisitiza juu ya umuhimu wa kuendeleza kumbukizi ya tukio hili la kihistoria katika fikra na nyoyo za umma wa kiislamu Duniani kote
Maoni yako